Mhubiri 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mhubiri 3 (Swahili) Ecclesiastes 3 (English)

Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Mhubiri 3:1

For everything there is a season, and a time for every purpose under heaven:

Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; Mhubiri 3:2

A time to be born, And a time to die; A time to plant, And a time to pluck up that which is planted;

Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; Mhubiri 3:3

A time to kill, And a time to heal; A time to break down, And a time to build up;

Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza; Mhubiri 3:4

A time to weep, And a time to laugh; A time to mourn, And a time to dance;

Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; Mhubiri 3:5

A time to cast away stones, And a time to gather stones together; A time to embrace, And a time to refrain from embracing;

Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa; Mhubiri 3:6

A time to seek, And a time to lose; A time to keep, And a time to cast away;

Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; Mhubiri 3:7

A time to tear, And a time to sew; A time to keep silence, And a time to speak;

Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani. Mhubiri 3:8

A time to love, And a time to hate; A time for war, And a time for peace.

Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo? Mhubiri 3:9

What profit has he who works in that in which he labors?

Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. Mhubiri 3:10

I have seen the burden which God has given to the sons of men to be afflicted with.

Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho. Mhubiri 3:11

He has made everything beautiful in its time. He has also set eternity in their hearts, yet so that man can't find out the work that God has done from the beginning even to the end.

Mimi najua ya kwamba hakuna jema kwao kupita kufurahi, na kufanya mema maadamu wanaishi. Mhubiri 3:12

I know that there is nothing better for them than to rejoice, and to do good as long as they live.

Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote. Mhubiri 3:13

Also that every man should eat and drink, and enjoy good in all his labor, is the gift of God.

Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye. Mhubiri 3:14

I know that whatever God does, it shall be forever. Nothing can be added to it, nor anything taken from it; and God has done it, that men should fear before him.

Yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako; naye Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita. Mhubiri 3:15

That which is has been long ago, and that which is to be has been long ago: and God seeks again that which is passed away.

Zaidi ya hayo, nikaona tena chini ya jua ya kwamba, Mahali pa hukumu upo uovu, Na mahali pa haki upo udhalimu. Mhubiri 3:16

Moreover I saw under the sun, in the place of justice, that wickedness was there; and in the place of righteousness, that wickedness was there.

Nikasema moyoni mwangu, Mungu atawahukumu wenye haki na wasio haki; kwa kuwa kuna wakati huko kwa kila kusudi na kwa kila kazi. Mhubiri 3:17

I said in my heart, "God will judge the righteous and the wicked; for there is a time there for every purpose and for every work."

Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama. Mhubiri 3:18

I said in my heart, "As for the sons of men, God tests them, so that they may see that they themselves are like animals.

Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. Mhubiri 3:19

For that which happens to the sons of men happens to animals. Even one thing happens to them. As the one dies, so the other dies. Yes, they have all one breath; and man has no advantage over the animals: for all is vanity.

Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena. Mhubiri 3:20

All go to one place. All are from the dust, and all turn to dust again.

Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini? Mhubiri 3:21

Who knows the spirit of man, whether it goes upward, and the spirit of the animal, whether it goes downward to the earth?"

Hivyo nikaona ya kwamba hakuna jema kupita mwanadamu kuzifurahia kazi zake; kwa sababu hili ni fungu lake; kwa maana ni nani atakayemrudisha tena ili ayaone yatakayomfuata baadaye. Mhubiri 3:22

Therefore I saw that there is nothing better, than that a man should rejoice in his works; for that is his portion: for who can bring him to see what will be after him?